Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano linalomulika biashara na haki za binadamu kufanyika Colombia

Kongamano linalomulika biashara na haki za binadamu kufanyika Colombia

Zaidi ya wajumbe 400 kutoka sekta mbalimbali duniani watakutana kwa kongamano la kwanza la Amerika Kusini na Caribbean lenye shabaha ya kujadilia namna biashara inavyoweza kuathiri haki za binadamu.

Baadhi ya wajumbe kwenye kongamanohilo wanatazamiwa kutoa taasisi za kiserikali, mashirika ya kiraia, vyama vya kibiashara na wasomi wa kanda mbalimbali.

Kongamano hilo ambalo ni kubwa kuwahi kufanyika limeandaliwa kwa ushirikiano wa pamoja baina ya Umoja wa Mataifa na kupitia kitengo cha biashara na haki za binadamu na shirika la maendeleo UNDP kanda ya Amerika Kusini.

Limepangwa kufanyika katika mji wa Medellín huko Colombikuanzia August 20 hadi 30 mwaka huu.