Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Syria yaridhia uchunguzi kwenye eneo la Ghouta linalodaiwa kutumika silaha za kemikali

Syria yaridhia uchunguzi kwenye eneo la Ghouta linalodaiwa kutumika silaha za kemikali

Hatimaye serikali ya Syria imekubali wakaguzi wa Moja wa Mataifa walioko nchini humo kuchunguza eneo ambalo tarehe 21 mwezi huu linadaiwa kutumika silaha za kemikali.

Taarifa ya msemaji wa umoja wa mataifa iliyotolewa Jumapili imesema wakaguzi hao wakiongozwa na Profesa Alke Sellstrom wataanza kazi hiyo kesho Jumatatu na uamuzi huo unafuatia mazungumzo kati ya serikali ya Syria na mwakilishi wa ngazi ya juu wa umoja huo kuhusu kuzuia kuenea kwa silaha Angela Kane mjini Damascus.

Tayari Katibu Mkuu Ban Ki-Moon ametaka jopo hilo kujikita zaidi kwenye uchunguzi huko Ghouta na kutambua taarifa kutoka Syria kuwa itatoa ushirikiano wa kutosha ikiwemo kuepusha chuki zaidi kwenye eneo hilo litakalofanyiwa uchunguzi.

Halikadhalika ameshukuru ushirikiano kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kupiga marufuku matumizi ya silaha za kemikali na shirika la afya duniani, WHO.