UM wapongeza miaka kumi ya mkataba wa amani Liberia:

21 Agosti 2013

Maafisa wa ngazi za juu wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani Liberia wamewapongeza watu na serikali ya Liberia kwa kudumisha amani kwa zaidi ya miaka kumi sasa na kuwataka washiriki ya kawaida wakizuia kurejea kwa machafuko kama siku za nyuma. Taarifa ya Alice Kariuki inafafanua zaidi:

(TAARIFA TA ALICE KARIUKI)

Katika taarifa yake Mkuu huyo Karin Landgren,amesema kuwa wakati wananchi wa Liberia wakijumuika pamoja kuadhimisha miaka kumi ya utulivu na amani, ni wajibu wa kila raia kuhakikisha anajiweka kando na mambo yanayoweza kurudisha nyuma maendeleo yaliyofikiwa.

Pamoja na kutolewa wito huo, mtaalamu huyo wa Umoja wa Mataifa amemtumia salama za pongeza rais  Ellen Johnson Sirleaf na serikali yake kwa kufanikisha mchakato wa amani na hatimaye taifa hilo sasa linapiga hatua kusonga mbele

 Sherehe hizo za kuadhimisha miaka 10 ya amani na utulivu zilipambwa na shughuli mbalimbali ikiwemo umati mkubwa wa watu waliojitokeza bara barani huku wakiwa wamebeba bendara ya taifa yenye rangi nyekundu,nyeupe na bluu.