Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulinzi wa raia kwenye mizozo bado ni changamoto, Ban ataka hatua zaidi

Ulinzi wa raia kwenye mizozo bado ni changamoto, Ban ataka hatua zaidi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu ulinzi wa raia kwenye mizozo ambapo Katibu Mkuu Ban Ki-Moon amesema ulinzi wa raia unabakia kuwa moja ya mambo ya msingi kwa operesheni Tisa za ulinzi wa amani za umoja huo. Bwana Ban amesema hayo wakati wa mjadala wa wazi wa baraza la usalama kuhusu ulinzi wa raia kwenye migogoro akigusia mizozo inayoendelea ikiwemo katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambayo amesema inatia raia mashakani.

(Sauti ya Ban)

Huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, raia wakiwemo watoto wanakumbwa katika mapigano, wanakumbana na ukatili wa kingono na kijinsia, wanauawa na hata kutumikishwa kwa nguvu na kushikiliwa. Ukiukwaji huu umefanyika muda mrefu. Nazisihi pande zote kuwajibika kwa mujibu wa sheria ya kimataifa na kutekeleza makubaliano ya amani, ulinzi na ushirikiano kwa DRC na ukanda wote. Ulinzi wa raia unahitaji hatua za kisiasa na kuwalinda.”

Mratibu Mkuu wa usaidizi wa kibinadamu ndani ndani ya Umoja wa Mataifa, OCHA, Valerie Amos akizungumza kutoka Brazil amesema usaidizi wa kibinadamu bado unakumbana na vikwazo akigusia Syria ambako amesema hali bado si shwari, misaada haiwafikii walengwa, licha ya vikwazo.

(Sauti ya Valerie Amos)

Mzozo wa Misri nao ulichomoza kwenye mjadala huo kupitia Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay ambaye amesema kiwango cha ukiukwaji wa haki za binadamu kwenye maeneo ya mizozo ni kikubwa kupita kiasi akitaka kuzingaiwa kwa sheria za kimataifa na wahusika wawajibishwe.

(Sauti ya Pillay)