Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia yahitaji misaada zaidi ya kibinadamu: OCHA

Dunia yahitaji misaada zaidi ya kibinadamu: OCHA

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya utoaji wa misaada ya kibinadamu, Umoja wa Mataifa na wabia wake zikiwemo kampuni, wamechochea kampeni ijulikanayo dunia yahitaji zaidi ikiwa na lengo la kuhamasisha usaidizi wa watu waliokumbwa na majanga ya kibinadamu.

Ofisi ya Umoja wa kimataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA imesema ni dhahiri ya kwamba dunia yahitaji utu zaidi ambapo mwaka huu pekee mashirika ya misaada yamesaidia watu zaidi ya Milioni 70, lakini usaidizi wahitajika zaidi. Matthew Cochraine ni msemaji wa OCHA kwa siku hii ya kimataifa.

(Sauti ya Matthew Cochraine)