Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka Misri kutumia njia mpya katika kupata suluhu la kisiasa nchini humo

Ban ataka Misri kutumia njia mpya katika kupata suluhu la kisiasa nchini humo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ban Ki Moon ameelezea hisia zake kutokana na jinsi hali ilivyo nchini Misri na kutoa wito kwa pande zote husika kuachana na uchokozi na kutumia njia ziingine kuhakikisha kuwepo kwa mapatano. Kupitia kwa msemaji wake Ban amesema kuwa ataunga mkono harakati zote zisizoshirikisha ghasia zenye lengo la kutimiza mahitaji ya wananchi wa Misri.

Misri imeshuhudia mabadiliko ya kisiasa tangu kupinduliwa kwa rais Hosni Mubarak miaka miwili iliyopita baada ya kushuhudiwa kwa maandamano makubwa. Mwezi uliopia watu kadha waliuawa na wengine wakajeruhiwa ambapo jeshi la Misri lilimuondoa madarakani rais Mohamed Morsy. Ban amepongeza jitihada za wananchi wa Misri kwa kipindi chama miaka kiwili iliyopita ambapo wamepigania haki ya ya kukusanyika na kujieleza kwa lengo la kuipeleka mbele nchi hiyo.