Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaiomba serikali ya Sudan kutoa vibali kwa wafanyikazi wake Darfur

UNHCR yaiomba serikali ya Sudan kutoa vibali kwa wafanyikazi wake Darfur

 

 

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, limetoa wito kwa serikali ya  Sudan itoe vibali vya kufanya kazi kwa wafanyakazi wake 20 wa kimataifa katika jimbo la Darfur, ambao waliamrishwa kuondoka nchini humo mwanzoni mwa mwezi Julai. Alice Kariki na taarifa kamili.

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

UNHCR inasema kuwa serikali ya Sudan imekataa kuwaongezea muda wa kufanya kazi wafanyikazi hao, wengi waliokuwa wakihudumu kwenye eneo la El Fasher Kaskazini mwa jimbo la Darfur. UNHCR inasema kuwa hata baada ya kulifuatilia suala hilo hakuna sababu yoyote iliyotolewa na serikali kuhusu ni kwa sababu gani muda wa wafanyikazi hao hukuongezwa. Msemaji wa UNHCR Melissa Fleming anasema kuwa kupunguzwa kwa idadi ya wafanyikazi kumesababisha kupungua kwa huduma za Shirika hilo hasa huduma kwa wakimbizi wa ndani kaskazini mwa Darfur.

(SAUTI YA MELISA FLEMING)

Leo tunatoa wito kwa serikali ya Sudan kuongeza muda wa kufanaya kazi kwa wafanyikazi wa UNHCR walio Darfur. Tuanahitaji kuwa uko kuendelea na kazi zetu za usalama kuwasaidia maelfu ya watu waliohama makwao eneo hilo. Darfur pekee watu milioni 1.2 wanaishi kwenye kambi. Kwa mwaka huu pekee tuna wakimbizi wa ndani wapya 300,000, theluthi moja kati yao au lakini moja wakiwa kaskazini mwa Darfur ambapo hatutatoa huduma jinsi tunataka na hata kama tumetoka kuna washirika kadha wanaofanyakazi nasi ambao hawajaathiriwa.

Anasema kuwa UNHCR ina jumla ya wafanyikazi 37 kwenye jimbo la Darfur lakini ni 17 tu ambao wana vibali vya kuwaruhusu kuendelea kufanya kazi.