Ofisi ya haki za binadamu yashangazwa na sheria nchini Bahrain
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imetiwa wasi wasi na mapendekezo yaliyotolewa na bunge la Bahrain waki wakati wa kikao kilichoandaliwa kujadili kuwaongezea adabu wale wanaohusika kwenye ugaidi. Mapendekezo hayo yanahusu kuongezwa kwa kifungo au kutupiliwa mbali kwa uraia kwa yeyote ambaye atapatikana na makosa ya kuhusika kwenye ugaidi mapendekezo ambayo yanapiga marufuku mikutano kwenye mji mkuu Manama.Tarehe 31 mwezi uliopita amri ya kutaka kurekebishwa kwa sheria hiyo kuambatana na mapendekezo hayo ilitolewa. Ofisi ya haki za binadamu hata hivyo inasema kuwa ni jukumu la kila nchi kuhakikisha kuwa sheria imetekekelezwa ikikukumbukwa kuwa hatua yoyote ni lazima iheshimu viwango vya haki za binadamu vya kimataifa. Cécile Pouilly ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.
(SAUTI YA CECILE POUILLY)