Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNFPA yajikita kupambana na ukeketaji Uganda

UNFPA yajikita kupambana na ukeketaji Uganda

Baada ya shirika la afya duniani , WHO, kutoa ripoti inayoonyesha hali ya ukeketaji barani Afrika na Mashariki ya mbali katika ukanda wa Afrika Mashariki Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa idadi ya watu UNFPA unaendelea na juhudi za kuelimisha jamii juu ya namna ya kuepuka kitendo hicho haramu.

Akiongea kutoka nchini Uganda Afisa wa jinsia wa UNFPA Christine Kwayu kutoka Tanzania ambaye amesema japo kitendo hicho ni cha kiimani lakini harakati zinaendelea kuleta tofauti.

(SAUTI CHIRSTINE)

Katika hatua nyingine Bi Kwayu amesema chini Uganda wanawake wanakumbana na madhila kadhaa ya kijinsia ikiwamo ndoa za umri mdogo pamoja na vipigo na kwamba UNFPA imejikita katika kuelimisha jamii kuondokana na ukatili huo wa kijinsia.

(SAUTI CHRSTINE )