Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biashara ya huduma duniani robo ya kwanza ya 2013, bara la Asia lachanua

Biashara ya huduma duniani robo ya kwanza ya 2013, bara la Asia lachanua

Toleo jipya la takwimu kuhusu biashara ya kimataifa katika sekta ya huduma kwa robo ya pili ya mwaka huu linaonyesha ongezeko la biashara hiyo kwa asilimia nne ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana ambapo bara la Asia na Oceania ndiyo yaliyopigia chepuo ongezeko hilo. Takwimu hizo za pamoja za Kamati ya biashara na maendeleo duniani, UNCTAD na shirika la biashara duniani, WTO zinahusisha mwezi Januari hadi Aprili zimedhihirisha ukuaji wa biashara ya dunia baina ya mataifa duniani.

Katika ukuaji huo bara la Asia na Ocenia limechangia asilimia Tano, Amerika ya Kaskazini asilimia Nne ilihali bara la Ulaya ni asilimia tatu wakati huu ambapo uchumi wao unaibuka kutoka kwenye mdororo. Toleo hilo linataja sababu za kudorora kwa biashara ya kimataifa ya huduma mwaka jana kuwa ni kudhoofika kwa uchumi wa bara la Ulaya ambao sasa unaibuka. Biashara za huduma husika ni kama vile teknolojia ya mawasiliano, bima na ushauri kwenye kandarasi.