Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghana yatakiwa kulinda haki wakati uchumi ukikua:UM

Ghana yatakiwa kulinda haki wakati uchumi ukikua:UM

Serikali ya Ghana imetakiwa kuandaa uchumi wake , jamii na taasisi ili kuhakikisha kwamba ukuaji wa uchumi wake hautoathri ulinzi wa haki za binadamu limeonya kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu biashara na haki za binadamu.Alexandra Guaqueta amesema ukuaji haraka wa uchumi unaweza kusababisha changamoto katika kulinda haki. Ameyasema hayo katika mwisho wa ziarayaoya siku 10 nchiniGhana.

Ameongeza kuwa wawekezaji wa kitaifa na kimataifa wanahitaji kuonyesha mfano wa kuheshimu haki za binadamu wakati wakishiriki katika ukuaji wa uchumi wa taifa hilo.

Bi Guaqueta na mwenzake Pavel Sulvandziga wameitaka serikali ya Ghana kuhakikisha kwamba misingi ya Umoja wa Mataifa ya biashara na haki za binadamu inazingatiwa na kuwekwa katika sera mpya za majukumu ya kijamii ambazo zinaundwa na wizara ya biashara na viwanda.

Wataalamu hao wamesema Ghanaina mfumo imara wa kisheria unaoweza kulinda haki, hata hivyo sheria na kanuni za ajira ya watoto, afya na usalama, saa za kufanya kazi na ubaguzi dhidi ya wanawake wakati wa ajira mara nyingi hazitekelezwi na sekta za biashara wala serikali.

Wamesema watui hususani vijijini na katika sekta isiyo rasmi wanakabiliwa na vikwazo vya kupata haki kwenye mfumo wa sheria.