Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasomali wanaotoroka Yemen wawezeshwa: IOM

Wakimbizi wa Somalia walioko Yemen warejeshwa nyumbani. IOM inaendelea kuwawezesha wakimbizi ambao tayari wamerejea. Picha: IOM

Wasomali wanaotoroka Yemen wawezeshwa: IOM

Mgogoro unaoendelea nchini yemen umewafanya Wasomali waliokimbilia huko kurejea kwao. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linashughulika wahamiaji-IOM, mamia wengi wa raia hao wa Somalia wanarejea nyumbani kila uchao.

Ili kusaidia raia wanaorejea nyumbani kuweza kutulia na kuleta uwelewano na wale waliobaki, IOM imetoa vifaa vya kuvulia samaki na maboti kwa vyama vya ushirika vya wananchi mjini Mogadishu.

Vyama vidogo vitatu vya ushirika vinavyojumulisha wanachama 64, ambao wote ni wanaume, ndivyo vilifaidika na msaada huo, kwa usaidizi wa wizara ya nje ya Marekani.

Vyama hivyo vimegawanywa katika mafungu matatu: wasomali wanaorejea kutoka Yemen; jamii ya wenyeji na tatu ni ya wale waliopoteza makazi yao.

Mwenyekiti wa chama kimoja cha ushirika, Mohamen Osman anasema kuwa wamekuwa wakigawana vifa vichache walivyokuwa nao na ndugu zao wanaorejea kutoka Yemen bada ya kugundua kuwa walikuwa wavuvi wazuri na kutokana na msaada huu sasa tuna vifaa vya kutosha kusaidia biashara yao.

Mmoja wa wasomali waliorejea amebaini kuwa kuwepo kwake kama mwanachama wa chama cha ushirika cha uvuvi kimemletea matumaini ya kuendelea na biashara yake ya uvuvi aliokuwa nayo nchini Yemen, na kuongeza kuwa msaada wa IOM umewaongezea matumaini kutokana na changamoto waliokuwa nazo mfano wa kuwa na vitendea kazi vichache.

Yeye naibu mwenyekiti wa chama kingine cha ushirika, ambae pia nae ndio karejea kutoka Yemen, amesema amejawa na furaha kwani mzigo wa wavuvi wa eneo hilo umepunguzwa na kuongeza kuwa sasa wanamatumaini makubwa kuwa biashara yao itashamiri na hivyo kuishukuru IOM kwa msaada uliokuja wakati muafaka.

Miongoni mwa vitendea kazi vilivyotolewa na IOM kwa jamii hizo ni kama vile, boti, injini za mataboti, maboya okozi, nyavu na vitu vingine vingi.Vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa wenyeji Disemba 17, mwaka 2017.