Zaidi ya wahamiaji 8000 wameingia nchini Italia mwaka huu

5 Julai 2013

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linakadiria kuwa takriban wahamiaji 8,400 na watafuta hifadhi waliingia kwenye pwani ya Italia katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka huu. Jason Nyakundi anaripoti.

(TAARIFA YA JASON NYKUNDI)

Wengi wa wale waliofanya safari hii walitoka maeneo ya Kaskazini mwa Afrika hususan nchini Libya ambapo walitoka watu 6700. Wengine 1,700 waliosalia walitoka nchini Ugiriki na Uturuki na kuingia maeneo ya kusini mwa Italia ya Apulia na Calabria. Karibu watu 7,800 waliingia nchini Italia huku Malta ikipokea karibu wahamiaji 600 wakiwemo watafuta hifadhi. Nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara ndiko wengi wa wahamiaji hawa hutoka hasa nchini Somalia na Eritrea. Mataifa mengine wanakotoka wahamaijai hawa ni Misri, Pakistan na Syria. Raia wa Gambia, Mali na Afghanistan pia hufanya safari hii lakini kwa viwango vya chini . Adrian Edwards msemaji wa UNHCR anafafanua zaidi.

(CLIP YA ADRIAN EDWARD)