Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukanda wa Afrika wapiga hatua utekelezaji MDG: Ban

Ukanda wa Afrika wapiga hatua utekelezaji MDG: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara umepiga hatua yakinifu katika kutekeleza malengo ya mendeleo hayo hususani katika elimu, afya, mapambano dhidi ya malaria na kifua kikuu. Kama inavyofafanua taarifa ya Jason Nyakundi

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)

Malengo manane ya milenia yalohusu ufukara, njaa, usawa wa jinsia, afya, elimu na mazingira, yalifiafikiwa na nchi zotekamamatokeo ya kongamano la Umoja wa Mataifa la milenia mnamo mwaka 2000, na tarehe ya kutimiza malengo hayo ikakubaliwa kuwa mwaka 2015.

Ripoti ya MDG mwaka 2013 inasisitiza kuwa hatua zimepigwa katika kufikia malengo kwa ajili ya watoto wote kusini mwa Jangwa laSahara. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ukanda huo uliongeza maradufu viwango wastani vya kupunguza vifo vya utotoni kutoka asilimia 1.5 kila mwaka kati ya 1990 na 2000, hadi asilimia 3.1 kila mwaka kati ya mwaka 2000 na 2011, ingawa ukanda huo bado unaongoza katika idadi ya vifo vya utotoni. Vifo vya watoto chini ya miaka mitano vilipungua kwa asilimia 39.

Ripoti pia inasema hatua zimepigwa katika kuongeza upatikanaji wa elimu ya msingi, huku idadi ya watoto wanaosajiliwa katika shule za msingi ikipanda kutoka asilimia 60 hadi asilimia 77 kati ya mwaka 2000 na 2011.

Hata hivyo, ukanda wa Kusini mwa Jangwa laSahara bado ndio ulioathiriwa zaidi na HIV na UKIMWI. Nimezungumza na baadhi ya wananchi waKenya kupata maoniyao kuhusu ripoti hii