Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lugha ya Kiswahili yazidi kung’ara medani za kimataifa: Balozi Kamau

Lugha ya Kiswahili yazidi kung’ara medani za kimataifa: Balozi Kamau

Baada ya kuzinduliwa huko Kilifi, Kenya wiki iliyopita, muhtasari wa ripoti ya Maendeleo ya binadamu kwa mwaka 2013 katika lugha ya Kiswahili iliwasilishwa rasmi mjini New York, Marekani na kushuhudiwa na wageni mbali mbali ikiwemo wawakilishi wa nchi za Angola, Burundi, Uganda, Tanzania na Kenya na Umoja wa Afrika katika Umoja wa mataifa.Ripoti hiyo inayoonyesha kuinuka kwa nchi za Kusini mwa inafanyia tathmini hatua za maendeleo zilizopigwa duniani kote, changamoto zinazojitokeza na nafasi zinazoibuka za utawala shirikishi.

Mwakilishi wa kudumu wa Kenya katika Umoja wa Mataifa Balozi Macharia Kamau amezungumzia uzinduzi huo.

SAUTI YA Balozi MACHARIA)

Taarifa zaidi juu ya uzinduzi wa ripoti hiyo itawajia katika makala yetu ya wiki ambayo pia itapatikana katika tovuti yetu.