Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Adha ya ukimbizi sio kwa mtu mmoja tuu bali ni kwa

Adha ya ukimbizi sio kwa mtu mmoja tuu bali ni kwa

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi na dunia nzima kwa ujumla wanaadhimisha siku ya wakimbizi duniani kwa kupongeza ushupavu na na ushujaaa wa watu zaidi ya milioni 40 duniani ambao wamelazimika kufungasha virago kutokana na vita au mauaji. Flora Nducha na taarifa kamili.

 (RIPOTI YA FLORA NDUCHA)

Kauli mbiu ya mwaka huu ni familia moja, kampeni ambayo ina lengo la kuikumbusha dunia kwamba wahanga wa vita ni kina mama, kina baba, na watoto wavulana kwa wasichana, na kwamba familia moja ikisambaratishwa na vita ni watu wengi mno. Akitoa ujumbe maalumu kuhusu siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema vita vinasalia kuwa sababu kubwa inayowafanya watu kukimbia makwao akitolea mfano wa machafuko yanayoendeleaSyria. Ban amesema zaidi ya nusu ya wakimbizi walioorodheshwa kwenye ripoti ya kamisha mkuu wa wakimbizi Antonio Guterres wanatoka katika nchi tano zilizoghubikwa na vita ambazo ni Afghanistan, Somalia, Iraq, Syria na Sudan. Akizitaja zingine zilizoathirika kuwa niMalina Jamhuri ya Kidemokrasia yaCongo. Naye mkuu wa UNHCR nchini Tanzania Joyce Mends-cole yeye anazungumzia hali ya familia kwenye kambi ya Nyarugusu nchini humo na anasema..  

(SAUTI YA JOYCE MENDS-COLE)