Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania na harakati za kutokomeza ajira za watoto majumbani

Tanzania na harakati za kutokomeza ajira za watoto majumbani

Wiki hii dunia iliadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza ajira za watoto. Siku hiyo ilifanyika huku mkutano wa kimataifa wa 102 wa shirika la kazi duniani, ILO ukiendelea hukoGeneva, Uswisi. Maudhui ya mwaka huu ni kutokomeza ajira za watoto majumbani. ILO inasema kuwa watoto zaidi ya Milioni 10 na nusu wameajiriwa majumbani duniani kote na wengine wana umri wa hata miaka mitano na idadi kubwa ni watoto wa kike. Ajira hizo zinawanyima hakiyaoya msingikamaile ya kuendelezwa inayojumuisha pia kupata elimu. Je nchiniTanzaniahaki iko vipi? Ungana basi na George Njogopa katika makala hii.