Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

NGO's zisiwekewe kisasi, Urusi,wataalamu:UM

NGO's zisiwekewe kisasi, Urusi,wataalamu:UM

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamekosoa vikali hatua ya serikali ya Russia kuyatia kwenye mashtaka mashirika mawili yasiyo ya kiserikali ambayo yalitoa ushahidi kuhusiana na vitendo vya mateso vilivyofanywa na Russia. 

Mashirika hayo ikiwemo kituo kinachopinga ubaguzi kilichopo St Petersburg  na Wakfu wa hukumu ya umma, yalitiwa hatiani katika kipindi cha mwezi April na May kwa makosa ya kwenda kinyume na hati ya kuandikishwa kwao kwa kile kilichoelezwa kuwa kujihusisha na shughuli za kisiasa.Mwenyekiti wa kamati inayopinga vitendo vya utesaji Claudio Grossman pamoja na mwenyekiti wa kamati ya utoaji wa fidia George Tugushi wamesema kuwa wamepata taarifa inayosema kuwa kitendo chao cha kutoa ushahidi kimechukuliwa kama msingi wa mashtaka dhidi yao.

Wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa wameikumbusha mamlaka ya Russia kuwa hatua yoyote inayoweza kuchukuliwa na dola juu ya vitendo vya utesaji itakuwa inakwenda kinyume na Mkataba wa Kimataifa unapinga vitendo vya utesaji mkataba ambao Russia imeuridhia.