Ukatili DRC umekithiri na umepitiliza: Kang

31 Mei 2013

Naibu Mkuu wa ofisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu ndani ya Umoja wa Mataifa, OCHA, Kyung-wha Kang, amehitimishia ziara yake ya siku nne huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC katika kijiji cha ndani zaidi cha Mulamba jimbo la Kivu Kusini na kusema ukatili umekithiri na umevuka mpaka. Taarifa ya Grace Kaneiya na maelezo zaidi.

(TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

Bi Kang alikutana na wawakilishi wa jamaa waliokosa makazi pamoja na jamii ya watu wengine ambao daimu wametoa wito wa kuwepo kwa amani.

Akiwa kwenye kituo kinachotumika kwa ajili ya usambazaji wa chakula, Kang a.likutana na kuzungumza na mama mmoja ambaye hali ya maisha yake ilikuwa mbaya na alikuwa akihitaji msaada wa dharura kuinusuru familia yake ambayo pia ilikuwa imekosa makazi.

Akiwa Kivu Kusin, alitembelea hospitali ya Panzi iliyojo mjini Bukavu ambayo iliasisiwa na Dr Denis Mukwege. Hospitali hiyo inajihusisha zaidi na matibabu kwa wale wenye matatizo ya kisaikolojia na inatoa msaada wa kisheria kwa wanawake na wasichana ambao ni manusuru wa ubakaji na unyanyasaji wa kingono.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter