Sasa kazi ni kujielekeza kwenye utekelezaji wa mkataba wa amani huko DRC: Ban

29 Mei 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema jambo muhimu hivi sasa ni kuangalia utekelezaji wa mkataba wa amani, usalama na ushirikiano katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC na kwamba ushiriki madhubuti wa nchi nyingi kwenye mchakato huo utaleta amani huko Maziwa Makuu.

Bwana Ban amesema hayo wakati akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kufahamu msimamo wa Umoja wa Mataifa juu ya hadhi ya baadhi ya vikundi ambavyo inadaiwa Tanzania imependekeza viingie kwenye mashauriano na Rwanda kama njia ya kuleta amani.

(SAUTI YA BAN)

Halikadhalika Bwana Ban amesema suala la maendeleo katika ukanda wa Maziwa Makuu litakuwa moja ya mambo atakayojadili katika mkutano wa Tano wa Tokyo kwa maendeleo ya Afrika, TICAD utakaoanza huko Yokohama, Japani mwishoni mwa wiki hii.

Bwana Ban alizungumza na waandishi wa habari mjini New York, baada ya kulipatia baraza la usalama muhtasari wa ziara yake huko Urusi na barani Afrika.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter