Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunaimarisha ulinzi kwa walinda amani: Ban

Tunaimarisha ulinzi kwa walinda amani: Ban

Wakati dunia inaadhimisha siku ya walinda amani duniani hii leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema Umoja huo kamwe hautasahau gharama za kijamii ambazo familia inakumbana nazo pindi jamaa au ndugu zao wanapojitolea mhanga kulinda amani duniani. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.(Taarifa ya Assumpta)

Kumbukumbu maalum ya walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa waliopoteza maisha yao sehemu mbali mbali duniani wakitetea misingi ya Umoja huo iliongozwa mjini New York, na katibu Mkuu Ban Ki-Moon.

Baada ya dakika moja ya ukimya, alizungumza na kueleza kuwa tangu kuanza Umoja wa Mataifa uanze kupeleka walinzi wa amani miaka 65 iliyopita, walinda amani Elfu Tatu wamekufa kwa sababu mbali mbali na mwaka jana pekee waliokufa ni 111.

Bwana Ban pamoja na kutuma rambirambi kwa familia na jamaa, amesema wanachofanya sasa ni kuimarisha ulinzi wa watendaji hao duniani kote.

(SAUTI YA BAN)

Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazolinda amani chini ya Umoja wa Mataifa na hapa ni msemaji wa jeshi la Tanzania Kapambala Mgawe.

(SAUTI YA MGAWE)

Je walinda amani wenyewe wanasemaje? Kaneng Muro kutoka jeshi la polisi Tanzania alihudumu Darfur chini ya kikosi cha UNAMID.

(Sauti ya Kaneng)