Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mukhisa Kituyi wa Kenya ateuliwa kuwa Mkuu wa UNCTAD

Mukhisa Kituyi wa Kenya ateuliwa kuwa Mkuu wa UNCTAD

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amemteua Mukhisa Kituyi wa Kenya kuwa Katibu Mkuu mpya wa Kamati ya Biashara na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD, kwa kipindi cha miaka minne, kuanzia Septemba mosi mwaka huu. Katibu Mkuu wa sasa Supachai Panitchpakdi anamaliza kipindi chake mwezi Agosti mwaka huu. Jason Nyakundi anaeleza zaidi.

TAARIFA YA JASON

Bwana Kituyi ni mbunge wa zamani kwenye bunge la Kenya na pia ashahudumu kama waziri wa biashara na viwanda nchini humo. Uteuzi huo utapelekwa kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuidhinishwa. Ikiwa ataidhinishwa bwana Kituyi anatachukua mahala pa Supachai Panitchpakdi kutoka Thailand ambaye amehudumu kwenye wadhifa huo tangu mwezi Septemba mwaka 2005 kabla ya kuteuliwa tena kwa marama ya pili mwaka 2009. Wakenya walikuwa na haya ya kusema kufuatia uteuzi huo.

(SAUTI)

Dkt. Mukhisa Kitui amezungumza katika mahojiano maalum na kituo hiki na kusema matarajio yake.