Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lengo sasa ni kumfikikishia kila mtu intaneti nafuu na salama: ITU

Lengo sasa ni kumfikikishia kila mtu intaneti nafuu na salama: ITU

Ulimwengu upo kwenye ncha ya mabadiliko, wakati mtandao wa intaneti unapohama kutoka kuwa soko kubwa katika nchi zilizoendelea na kupata ufuasi na matumizi makubwa kote duniani, amesema Hamadoun, Katibu Mkuu Shirika la Kimataifa la mawasiliano, ITU. Dr. Touré amesema hayo wakati wa kuhitimishwa kongamano la tano la kimataifa kuhusu sera za teknolojia ya mawasiliano, WTPF mjini Geneva, Uswisi leo.Dr Touré amesema kongamano hilo la WTPF limebuni mtazamo wa pamoja, ambao unaweza kugeuzwa kuwa hatua za kuchukuliwa ili kuwaunga thuluthi mbili ya watu kote duniani kwenye mtandao wa Intaneti, ili watu wote duniani wajumuishwe kwenye teknolojia hiyo ya mawasiliano.

Wawakilishi wa serikali, sekta binafsi na mashirika ya umma, wameshirikiana kupitia kongamano hilo, kwa lengo la pamoja la kuhakikisha kwamba kila mtu anawezeshwa kutumia intaneti yenye gharama nafuu na ambayo pia ni salama.