Ban na David Cameron wajadili Syria na ajenda baada 2015

15 Mei 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, na kumshukuru kwa uongozi wake na uungaji wake mkono kwa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala kadhaa, yakiwemo Somalia, Mali, wakimbizi wa Syria, kiwango cha msaada wa maendeleo unaotolewa na Uingereza na Mfuko wa Kimataifa kuhusu malaria, kifua kikuu na HIV, Global Fund.

Wamebadilishana mawazo kuhusu njia bora za kuzishawishi pande zinazozozana nchini Syria kutuma wajumbe wanaofaa kwa kongamano la kimataifa lililopendekezwa kwa ajili ya Syria, hasa wale ambao wako tayari kulegeza msimamo wao kuhusu suala la serikali ya mpito.

Viongozi hao wawili wamesema ushawishi kwa pande zote kutoka kwa jamii ya kimataifa ni muhimu. Pamoja na hayo, wameelezea umuhimu wa uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu madai ya matumizi ya silaha za kemikali. Pia wamejadiliana kuhusu Cyprus, na kuelezea umuhimu wa kutumia kipindi kijacho kupiga hatua za maendeleo nchini humo.Naye Bwana Cameron akizungumza na waandishi wa habari, alizungumzia majukumu aliyopewa yeye na viongozi wengine watatu duniani juu ya ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015.

Amesema baada ya mikutano ya London, Monrovia, Bali na hapa New York na wenzie Ellen Johnson Sirleaf na Susilo Bambang Yudoyono, wanaandaa ripoti ambayo itakuwa na mapendekezo makuu matatu juu ya ajenda baada ya mwaka 2015.  

Mapendekezo hayo ni pamoja na kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 umaskini uliokithiri unatokomezwa na huduma kama vile maji safi ya kunywa, afya, shule na  umeme vinapatikana kwa kila mtu. Pendekezo la pili ni.