Ujumbe wa UM Syria:UNICEF/WFP

14 Mei 2013

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamepeleka wajumbe wake kwenye eneo la Al-houle nchiniSyria, ambako zaidi ya watu 100, wakiwemo watoto 49, waliuawa katika machafuko, ndani ya kipindi cha siku moja mnamo Mei mwaka 2012.Huu ndio ujumbe wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kwenda katika eneo hilo, ambalo limekuwa halifikiki kwa miezi mingi tangu mapigano yalipoanza. George Njogopa na taarifa kamili

Pamoja na ujumbe huo, UNICEF pia imesambaza vifaa kwa ajili ya afya na usafi.Timu hiyo iliyotuma huko imebaini kuwepo kwa mapungufu makubwa ya vifaa vya kitabibu hatua ambayo imesababisha kushindwa kukabiliana na baadhi ya magonjwa yanayoripotiwa kwa wingi katika eneo hilo.

Miongoni mwa magonjwa hayo ni pamoja na tatizo la kuhara, magonjwa yanayoathiri mifumo ya upumuaji na magonjwa ya akili.

Pia kumekuwa na tatizo la uhaba wa huduma ya maji na maeneo mengine yanakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa mafuta kwa ajili ya kusuma mitambo ya maji.

Baadhi ya wauguzi wamesema kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wanaoandamwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo yale ya utapiamlo.

Marixie Mercado ni afisa kutoka UNICEF

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)

Na kwa upande wa timu kutoka shirika la chakula duniani WFP imewasili kwenye eneo hilo ikiwa na misaada mbalimbali ikiwemo mabehewa ya chakula chenye uwezo wa kuwatosha watu 25,000.Elizabeth Byrs wa WFP anaeleza zaidi.

(CLIP YA ELIZABETH BRYS)

Timu hiyo kwa pamoja imeshuhudia baadhi ya wanajamii ambao sasa wameanza kuzoe hali ya mambo ikiwa imeshoka kabisa.

Pamoja na kuwepo kwa shughuli za kilimo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, lakini eneo hil