Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna haja ya kuboreshwa kwa huduma za kijamii Iraq-UM

Kuna haja ya kuboreshwa kwa huduma za kijamii Iraq-UM

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq ametaka kuboreshwa kwa mazingira ya utoaji wa huduma za kijamii hasa kwa makundi ya wakimbizi wa ndani akisisitiza kuwa upatikanaji wa huduma hizo katika mazingira rafiki ni jambo linalopaswa kutekelezwa bila vikwazo vyovyote.

Amesema kuwepo kwa huduma bora kwa jamii ya wakimbizi wa ndani walioko kwenye kambi ya Al-Manar ni hatua muhimu na hasa wakati huu ambapo mahitajio yao yanaongezeka.

Mwanadiplomasia huyo , Martin Kobler,amesema huduma kama elimu unapaswa kuboreshwa na kutolewa katika mazingira ya uhalisia. Amesisitiza kuwa makundi ya watoto walioko kwenye eneo hilo wanapaswa kufikiwa na elimu itayowafanya wachangamane vyema na jamii zao nyingine.

Ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea makambi hayo yaliyoko nje kidogo ya mji wa Baghdad.