Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asisitiza utulivu wakati kukiripotiwa kutokea mashambulizi ya angani nchini Syria

Ban asisitiza utulivu wakati kukiripotiwa kutokea mashambulizi ya angani nchini Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa ameingiwa na wasiwasi kufuatia ripoti ya kufanyika kwa mashambulizi ya anga nchini Syria yaliyodaiwa kufanywa na ndege ya Israel.

Huku akisisitiza juu ya kile alichosema kuwa Umoja wa Mataifa bado hauna taarifa za moja kwa moja juu ya tukio hilo, Ban ametoa wito wa kujiepusha na hali yoyote inayoweza kuzorotesha usalama.

Ripoti za vyombo vya habari zimearifu mfululizo wa milipuko iliyojitokeza katika mji mkuu wa Damascus nyakati za asubuhi .

Televisheni ya Syria imesema kuwa mashambulizi hayo yameendeshwa na ndege ya Israel ambayo yalilenga kituo cha kijeshi. Hata hivyo Ban amesisitiza kuwa, Umoja wa Mataifa bado unafuatilia tukio hilo lakini amerejelea wito wa kuzingatia maazimio ya kimataifa.