Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu wa UM amelaani vikali mashambulio ya kigaidi nchini Iraq

Katibu Mkuu wa UM amelaani vikali mashambulio ya kigaidi nchini Iraq

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani mlolongo wa mashambulizi ya kigaidi nchini Iraq hapo jana, ambapo zaidi ya watu mia moja wameuwa huku wengine 350 wakijeruhiwa, na hivyo kulifanya tukio hilo kuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea mwaka huu.

Msemajiw a Umoja wa Mataifa Martin Nesirky ametoa taarifa kwa niaba ya Katibu Mkuu akisema, Katibu Mkuu amelaani vikali mashambulizi hayo ya jana, ambapo mamia ya watu wameuwawa na wengine wakijeruhiwa, wengi wao wakiwa raia . Na kuongeza kuwa Umoja wa Mataifa unaungana na wote walioathirika na kitendo hicho.

Kwa mujibu ya vyombo vya habari, mashambuzli hayo yalihusisha magari mawili ya bomu katika kiwanda cha kutengeneza nguo kilichoko katika eneo la Hila, mshambuliaji wa kujitoa mhanga katika soko lilokuwa na watu wengi katika mji mdogo wa Kusini mwa Baghdad, magari tatu katika mji wa Kusini, Basra, na magari mawili ya bomu katika mji wa Faluja na mashambuliaji mwingine kusini mwa Baghdad na Mosoul, mji mkuu mwa Kasakazini mwa Iraq.

(SAUTI Martin Nesirky: Katibu Mkuu amealaani vikali mashambulizi ya mabomu yaliyotokea jana nchini Iraq ambapo inaripotwa zaidi ya watu mia moja wameuwawa huku wengine wengi wakijeruhiwa, wengi wao wakiwa ni raia. Umoja wa Mataifa unaungana na raia wa Iraq katika wakati huu mgumu).