“Bodaboda” zalaumiwa kwa ongezeko la vifo vitokanavyo na ajali za barabarani Afrika

6 Mei 2013

Wakati wiki ya usalama barabarani ikiendelea kuadhimishwa sehemu mbalimbali duniani, mtaalamu wa masuala ya afya ya umma kutoka Chuo Kikuu cha Moi nchini Kenya Dokta Wilson Odero, amesema bara la Afrika lina idadi kubwa vifo vitokanavyo na ajali za barabarani na matumizi ya pikipiki au bodaboda yamesababisha ongezekohilo. Alice Kariuki na taarifa zaidi.

(ALICE TAARIFA)

Akizungumza kando ya kongamano la usalama barabarani lililoandaliwa na tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa barani Ulaya, Dokta Odero amesema takwimu za vifo vinavyosababishwa na ajali za barabarani huko Afrika ni za juu kuliko eneo lolote lile duniani. Mathalani amesema wakati takwimu za dunia zinaonyesha kuwa vifo Kumi naTisakati ya Laki Moja vyatokana na ajali barani Afrika idadi hiyo ni maradufu. Ametaja sababu kadhaa ikiwemo bodaboda.

(Dkt Odero)

“Afrika hivi sasa imeibuka kuwa soko la pikipiki za bei nafuu. Na hizi pikipiki sasa zimegeuzwa usafiri wa umma.  Ni wazi kuwa pikipiki hazijatengenezwa kwa ajili hiyo. Na si jambo la ajabu kuona abiria zaidi ya watatu au wanne kwenye pikipiki moja. Waendeshaji wa pikipiki hizi mara nyingi hawana mafunzo na wala hawana bima hivyo uendeshaji hovyo wa pikipiki sasa umekuwa mzigo mkubwa kwa nchi.