Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lafurahishwa na mazungumzo ya kitaifa Yemen

Baraza la Usalama lafurahishwa na mazungumzo ya kitaifa Yemen

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo wameelezea kufurahishwa na mazungumzo ya kitaifa yanayoendelea nchini Yemen, na ambayo yametajwa kuwa jumuishi. Mazungumzo ya kitaifa Yemen talianza mnamo Machi 18.

Kikao cha leo cha Baraza la Usalama pia kimehutubiwa na Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen, Ben Omar Jamal.

Kwa mujibu wa rais wa Baraza hilo kwa mwezi wa Aprili, Balozi Eugène-Richard Gasana wa Rwanda, hali nchini Yemen inaendelea kuimarika, licha ya kuwepo watu wanaojaribu kuvuruga mambo, hasa makundi ya kigaidi.