UNDP kukwamua wajasiriamali
Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, UNDP kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo umeanzisha mpango utakawawezesha wajasiriamali na sekta binafsi kwa ujumla kukuza kipato kwa haraka na kwa njia rahisi.
Mpango huo unaofahamika kama wito wa hatua za kibiashara ni mahususi kwa ajili ya kupambana na umaskini na unalenga zaidi kukuza vipato vya wajasiriamali wadogowadogo mathalani biashara ya kutuma hela kwa kupitia mitandao ya simu inayoshamiri kwa kasi barani Afrika.
Kwa mujibu wa Meneja wa mpango huo Sahba Sobhani jitihada hizo zitasaidia sekta binafsi katika kupambana na umaskini kwa kusaidia wajasiriamali kwa mifano njia sahihi za kupata masoko.
Miongoni mwa washirika wa kimaendeleo ktika mkakati huo ni Shirika la kimataifa la maendeleo laAustralia, Wizara ya mambo ya nje ya Uhollanzi pamoja na Shirika la Maendeleo la marekani USAID.