Wanasiasa wajadili mwelekeo wa uchaguzi mkuu Burundi: UM

11 Machi 2013

Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi, BNUB imeitisha kikao cha wanasiasa nchini humo kinachonuwia kumaliza uhasama na kuandaa  vema uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2015.

Kikao hicho kinawaleta  kwa pamoja wanasiasa walio karibu na chama tawala pamoja na wanasiasa wa upinzani ambao baadhi yao wamerejea nchini  wiki iliyopita. Katika mkutano huo wanasiasa hao wanajadili dosari zilizojitokeza katika  uchaguzi uliotangulia kama somo la kuangazia vema uchaguzi wa mwaka wa 2015. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametolea mwito  wanasiasa  hao  kuwa wazi kwenye mazungumzo yanayojenga ili kuchora mustakbali mzuri wa taifa la Burundi.

Mwandishi wetu wa Maziwa Makuu, Ramadhan Kibuga na ripoti kamili kutoka Bujumbura.

(SAUTI Ramadhani)