Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wa DRC wapaza sauti vita ikomeshwe

Wanawake wa DRC wapaza sauti vita ikomeshwe

Wakati dunia inaelekea katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mwanamke, baadhi ya wanawake kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC wanaoshiriki mikutano ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani kuhusu hali ya mwanamke, wamepaza sauti zao na kusema kuwa vita mashariki mwa nchi hiyo sasa basi kwani vinazidi kumgandamiza mwanamke na kumfanya ashindwe kupumzika.  Akizungumza katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa, mmoja wa wanawake hao Senakriste Goya amesema mapigano Mashariki mwa DRC yanawatumbukiza wanawake kwenye mazingira ya kikatili ikiwemo kubakwa na hivyo wanataka dunia ipaze sauti ili wakomboke.

(SAUTI YA Senakriste)