Wakimbizi wa Syria wafikia Milioni Moja: UNHCR

6 Machi 2013

Idadi ya raia wa Syria walio wakimbizi wa ndani na wa nje imeongezeka na kufikia milioni Moja, na hiyo ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR. Kamishna Mkuu wa UNHCR Antonio Guterres amesema idadi hiyo inaongezeka na kwamba wasyria wanaovuka mpaka inaongezeka kila siku. Guterres amesema hali ya Syria inakaribia kufikia janga kubwa kutokana na idadi kubwa ya watu kuachwa bila makaazi na kwamba hali hiyo lazima ikomeshwe. Amesema idadi hiyo ya Milioni Moja ina maana kwamba watu hao wanategemea ukarimu wa watu wanaowapokea, nchi jirani na mashirika ya misaada ya kibinadamu. Bwana Guterres amesema athari za idadi hiyo kwa nchi zinazowapokea ni mbaya. Msemaji wa UNHCR Adrian Edwards anaelezea hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa.

(SAUTI YA Adrian)