Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuendelea kwa mapigano Syria ni baa la kibinadmu la nyakati za sasa

Kuendelea kwa mapigano Syria ni baa la kibinadmu la nyakati za sasa

Naye Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Vuk Jeremic, amesema ufanisi wa mazungumzo kuhusu ustaarabu utatokana na jinsi masuala mawili sugu Mashariki ya Kati yanatatuliwa, ambayo ni janga la umwagaji damu Syria na hatma ya watu wa Palestina.

Akiongea kwenye kongamano hilo la nchi zinazoendeleza ustaarabu, Bwana Jeremic amesema, inasikitisha kuwa kwa takriban miaka miwili, jamii ya kimataifa imeshindwa kukomesha mauaji yaliyokithiri nchini Syria, katika mzozo ambao ameutaja kama baa la kibinadamu la enzi ya sasa.

Akisisitiza ujumbe wa haja ya wanadamu kuishi kwa amani, Bwana Jeremic amerejelea maandiko ya Qur’an na Biblia