Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya fanyeni uchaguzi kwa amani epukeni ukimbizi wa ndani: UM

Kenya fanyeni uchaguzi kwa amani epukeni ukimbizi wa ndani: UM

Ikiwa imesalia siku Tano kabla ya uchaguzi mkuu nchini Kenya Umoja wa Mataifa umeitaka nchi hiyo kuchukua tahadhari juu ya uwezekano wa kutokea vurugu zinazoweza kusababisha wakimbizi wa ndani wakati wa mchakato mzima wa uchaguzi. Ujumbe huo umetolewa na Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu wakimbizi wa ndani Chaloka Beyani ambaye amesema historia ya uchaguzi nchini humo inaonyesha kuibuka kwa wakimbizi wa ndani baada ya uchaguzi. Taarifa ya Joseph Msami inafafanua zaidi.

(SAUTI ya JOSEPH)