Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay ataka wavunjifu wa haki za binadamu Haiti kutokingiwa kifua

Pillay ataka wavunjifu wa haki za binadamu Haiti kutokingiwa kifua

Mahakama Kuu ya Rufani nchini Haiti inatazamia kuendelea juma hili kuzikiliza kesi dhidi ya vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu vilivyofanyika wakati wa utawala wa rais wa zamani wa nchi hiyo Jean-Claude Duvalier, Kamishna wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu Navy Pillay ameitolea mwito serikali kutowakingia kifua wale waliohusika na vitendo hivyo.  Pillay amesema kuwa serikali ya Haiti inapaswa kufahamu namna inavyowajibika kulinda na kutetea haku za binadamu na siyo kuendelea kuwatetea wavunjifu wa haki hizo. Kumekuwepo malalamiko juu ya baadhi ya makundi ya watu waliohusika na vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu lakini mamlaka za dola zimepuuza kuwafikisha mbele ya mkono wa sheria. Kwa upande mwingine, Kamishna huyo amepongeza juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na mahakama ambayo amesema kuwa zinachukua mkondo sahihi kushughulikia kesi za ukiukwaji wa haki za binadamu.