Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF kueneza mafanikio zaidi ya elimu jumuishi

UNICEF kueneza mafanikio zaidi ya elimu jumuishi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limetaja mafanikio zaidi yatokanayo na elimu jumuishi baada ya sera endelevu kuhusu mpango huo kuonyesha mafanikio makubwa katika nchi za Ulaya ya Kati na Mashariki pamoja na Asia ya Kati. Akizungumza na Radio ya UM mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Elimu Jumuishi, Paula Hunt amesema kuwa UNICEF ina mpango wa kuchukua mfano wa mafanikio haya na kuendeleza sera hizi katika maeneo yote ambako UNICEF inafanyia kazi.

(SAUTI YA PAULA HUNT)