Ban awasili Kuwait, atoa shukrani kwa maandalizi ya mkutano wa Syria

29 Januari 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon yuko nchini Kuwait tayari kushiriki mkutano wa wahisani kwa ajili ya Syria hapo kesho.

Tayari Bwana Ban amekuw ana mazungumzo na viongozi wa wa nchi hiyo akiwemo Mfalme wa nchi hiyo, Waziri Mkuu, Naibu Waziri Mkuu na waziri wa Mambo ya Nje.

Katika mazungumzo yao pamoja na kujadili hali halisi nchini Syria, Bwana Ban amewashukuru kwa jitihada zao za kuitisha mkutano huo wa wahisani kwa ajili ya Syria iliyoko katika mgogoro kwa sasa.

Amesema kitendo cha Kuwait kuandaa mkutano huo kimekuja wakati muhimu zaidi kwa Syria ambako hali ya kibinadamu inazidi kuzorota.

Katibu Mkuu ametambua pia jitihada dhahiri za Kuwait za kuunga mkono Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa hususan ukanda wa kiarabu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter