Mashirika ya UM yaungana na wadau kuzindua mkakati wa 'lisha mwili, lisha ubongo"

24 Januari 2013

Mashirika ya Umoja wa Mataifa kuanzia lile linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, shirika la mpango wa chakula duniani WFP na shirika la kuhudumia watoto UNICEF, yamekusanya nguvu kwa pamoja ili kuwasaidia mamia ya watoto wanaokabiliwa na hali ngumu.

Mpango huo wa miaka mitatu uliotangazwa kwenye kongamano la kitamaifa la uchumi linalofanyika Davos, Uswis unashabaha ya kuimarisha afya, utoaji wa lishe na eliumu kwa makundi ya watoto ambao hadi sasa bado hawajafikiwa na mahitaji hayo.

Kama sehemu yake ya kwanza ya majaribio, mpango huo utaanza kutekelezwa katika nchi za Haiti, Msumbiji, Niger na Pakistan. Taarifa kamili na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)