Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zerrougui asikitishwa na mauaji ya watoto yaliyofanywa na AMISOM

Zerrougui asikitishwa na mauaji ya watoto yaliyofanywa na AMISOM

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na migogoro ya kivita Leila Zerrougui amesema anasikitishwa sana na taarifa kuwa jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika nchini Somalia, AMISOM limeua watoto kadhaa wakati wa operesheni zake huko Shabelle siku ya Jumanne.

Ameeleza masikitiko yake wakati huu ambapo Kaimu Mkuu wa AMISOM Meja Jenerali Salvatore Harushimana, ameshatangaza kuwa atachunguza tukio hilo na mazingira yaliyosababisha kutokea.

Bi.  Zerrougui amesifu kitendo cha AMISOM kukiri kisa hicho na kuridhia kuchunguza ndani ya wakati na amesema ni matumaini yake uchunguzi huo utaibuka na matokeo thabiti ya kuepusha kutokea tena kaw kitendo hicho.

Halikadhalika ametaka walinda amani wa Umoja wa Afrika kutambua kuwa ulinzi wa watoto ni jambo muhimu katika operesheni zao zote ikiwemo Mali na maeneo yaliyoathiriwa na kikundi cha waasi cha Lord’s Resistance Army.