Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna cha kuhalalisha ugaidi: Ban

Hakuna cha kuhalalisha ugaidi: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema kamwe hakuna kitu chochote kinachoweza kuhalalisha ugaidi duniani. Hata hivyo amesema ni lazima kushungulikia mazingira yanayochochea vitendo hivyo.

Bwana Ban amesema hayo leo katika hotuba yake kwenye mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama juu ya mikakati ya kukabiliana na ugaidi duniani.

Amesema mashauriano baina ya jamii pamoja na kudhibiti misimamo mikali juu ya jambo fulani ni miongoni mwa hatua zinazoweza kuchukuliwa kudhibiti ugaidi.

Hata hivyo amesema hatua hizo zinawezekana iwapo mataifa mbali mbali na wananchi wenyewe watashiriki kuibuka na suluhisho la hatua stahili za kupambana na ugaidi. Amegusia suala la Mali ambako amesema ugaidi unatishia amani na kutaka Baraza la Usalama kushughulikia hali hiyo ipasavyo.

Mjadala huo wa wazi unaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Paksitani Hina Rabban Khar.