Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sayansi na Teknolojia yabakia ndoto kwa wanawake: ILO

Sayansi na Teknolojia yabakia ndoto kwa wanawake: ILO

Shirika la kazi duniani ILO linasema kuwa hatua zinastahili kuchukuliwa katika kutatua mwanya uliopo kweye uwakilishi wa wanawake kwenye nyanja za sayansi na teknolojia.

Claude Akpokavie afisa wa idara ya wafanyikazi ya ILO ACTRAV anasema kuwa hata kama maendeleo ya sayansi na teknolojia ni ya kasi, wanawake bado wanakabiliwa na hatari ya kuachwa nyuma.

Akpokavie ameandika makala kuhusu hatua zilizopigwa katika kuafikiwa kwa maendeleo ya malengo ya milenia ikiwemo usawa wa kijinsia na kuwainua wanawake ambapo amesema wanawake wana uwakilishi mkubwa kwenye masuala ya sayansi za kijamii ilhali wana uwakilishi mdogo kwenye sayansi na teknolojia.