Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtuhumiwa wa makosa ya uhalifu wa kivita DRC Mathiew Ngudjolo Chui hana hatia: ICC

Mtuhumiwa wa makosa ya uhalifu wa kivita DRC Mathiew Ngudjolo Chui hana hatia: ICC

Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC imeamuru kuachiwa huru kwa mtuhumiwa wa makosa ya uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu, Mathieu Ngudjolo Chui baada ya kumuona kuwa hana hatia.

Uamuzi huo umepitishwa kwa kauli moja na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Bruno Cotte kutoka Ufaransa ambapo wamesema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha madai dhidi ya mtuhumiwa na hivyo kuamuru msajili wa mahakama kuchukua hatua muafaka kumuachia huru Ngudjolo.

(SAUTI YA JAJI BRUNO COTTE)

Hata hivyo upande wa mashtaka unataka kukata rufaa na uamuzi utatolewa baadaye leo. Mathieu Ngudjolo Chui, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo alishtakiwa kwa makosa matatu ya uhalifu dhidi ya binadamu, na makosa saba ya uhalifu wa kivita ambayo anadaiwa kutenda wakati wa mgogoro huko Ituri mwezi Februari mwaka 2003.