Serikali zitekeleze ahadi za kulinda wanawake:Bachelet

28 Novemba 2012

Umoja wa Mataifa umezitaka serikali pamoja na viongozi mbali mbali duniani kutekeleza ahadi zao za kuhakikisha vitendo vyote vya unyanyasi dhidi ya wanawake vinatokomezwa, ambapo wito huo unatokana na ujumbe wa mwaka huu usemao Ahadi ni Ahadi.

Takwimu zinaonyesha kwa katika baadhi ya nchi wanawake kati ya Saba hadi Kumi hukumbwa na vitendo vya unyanyasaji kama vile kubakwa, kupigwa au kuuawa licha ya kuwepo kwa mikataba ya kimataifa na ya kikanda ya kuzuia vitendo hivyo.

Michelle Bachelet, ambaye ni Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya wanawke anasema changamoto zinazokabili wanawake bado ni nyingi iwe katika nchi maskini au zilizoendelea.

Unaweza ukaenda hata nchi zilizoendelea unyanyasaji wa wanawake upo na kwenye nchi zinazoendelea bila shaka ambapo vitendo vya dhuluma kwa misingi ya jinsia vimeshamiri, kuanzia majumbani, ndoa za lazima kwa watoto na hata ujauzito wa lazima, ukeketaji, usafirishaji wa binadamu, utesaji na ubakaji. Kwenye migogoro pia kuna vitendo vya unyanyasaji na hata migogoro inapomalizika bado unashuhudia unyanyasaji wa misingi ya kijinsia. Ni jambo gumu kwani hata makubaliano ya amani yanapofikiwa, vitendo vya dhuluma dhidi ya wanawake havimaliziki.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon na Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja huo kuhusu masuala ya wanawake, Michelle Bachelet hii leo wataongoza maadhimisho rasmi ya siku ya kutokomeza vitendo vya dhuluma dhidi ya wanawake duniani katika makao makuu mjini New York, Marekani huku umoja huo ukitambua kuwa vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wasichana na wanawake ni mojawapo ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyoshamiri dunia

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter