Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakazi wa Goma wahaha baada ya waasi wa M23 kutishia kufanya vurugu: OCHA

Wakazi wa Goma wahaha baada ya waasi wa M23 kutishia kufanya vurugu: OCHA

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kibinadamu, OCHA imesema hali ya usalama kwenye mji wa Goma ulioko Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRC ni mbaya kwa kuwa kikundi cha waasi cha M23 kimetishia kuingia na kufanya vurugu.

Afisa wa habari wa OCHA kwa DRC Yvon Edoumou amesema maelfu ya wakazi wa mji huo wamejawa na hofu na sasa wanahaha wakisaka maeneo yenye usalama na kwamba kambi moja ya watu walikombia makazi yao iliyokuwa na watu zaidi ya Elfu Sitini sasa ni tupu.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka mji mkuu wa DRC, Kinshasa, Edoumou amesema Umoja wa Mataifa unajaribu kuendelea kutoa msaada kwa watu hao licha ya kuzorota kwa hali ya usalama.

(SAUTI YA YVON EDOUMOU)