Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhifadhi wa mazingira wachomoza katika siku ya UM Tanzania

Uhifadhi wa mazingira wachomoza katika siku ya UM Tanzania

Nchini Tanzania, maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa yamefanyika jijini Dar Es Salaam ambapo shughuli mbali mbali zilifanyika kama vile makongamano, maonyesho na uhifadhi wa mazingira. George Njogopa na taarifa zaidi.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Maafisa wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania leo wameungana na wale wa serikali pamoja na raia wa kawaida kuadhimisha siku ya Umoja huo kwa kujishughulisha na mambo mbalimbali ikiwemo maonyesho ya wazi.

Kundi la watumishi wa Umoja huo wa Mataifa na kundi jingine la maafisa wa serikali ya Tanzania wakiongozwa na waziri wa ushirikiano wa afrika mashariki Samwel Sitta walikusanyika kwenye uwanja wa Karemjee ambako maadhimisho hayo yamefanyika kwa kushiriki kushughuli mbalimbali.

Bwana Austine Makani ambaye ni afisa habari wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi alisema kuwa , pamoja na mambo mengine lakini pia siku ya leo imeadhimishwa kwa kushiriki shughuli mbalimbali ikiwemo kutembelea maeneo ya kijamii.

Kwenye amadhimisho hayo mada nyingine iliyopewa uzito pia ni kutoa hotuba ambazo ziliangazia kuwapa msukumo watoto ili hatimaye kutimkiza ndoto zao.