Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji wa kimataifa wapungua mwaka 2012 UNCTAD

Uwekezaji wa kimataifa wapungua mwaka 2012 UNCTAD

Uwekezaji wa kigeni ulipungua kwa asilimia 8 kwenye miezi sita ya kwanza ya mwaka 2012 kutokana na misukosuko ya kiuchumi kwenye robo ya pili ya mwaka 2012. Ukuaji wa kujikokota wa uchumi duniani na hatari zinazotokana na kubadilika kwa sera kunayafanya makambuni mengi kuamua kutumia mbinu ya kusubiri na kuona yanapowekeza nje.

Katibu mkuu wa shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD Dr. Supachai Panitchpakdi anasema kuwa uwekezaji unachangia kukua kwa uchumi lakini mienendo iliyo sasa ya uwekezaji kwenye nchi zinazoendelea hasa Asia ni ya kuogofia na changamoto na kulekeleza uwekezaji wa kigeni kwenye sekta za kimaendeleoo zikiwemo za miundo msingi, kilimo na uchumi usioathiri mazingira zimesalia kuwa kubwa.