Bank ya dunia yatoa ripoti ya maendeleo 2011
Ripoti moja iliyotolewa na benki ya dunia imesema kuwa zaidi ya watu milioni 1.5 wanaishi katika nchi ambazo zinakabiliwa na mzunguko wa matukio yenye vurugu za kisiasa na uhalifu na hivyo maeneo hayo kutokana na kuharibiwa na machafuko kunatia shaka kama yanaweza kufikia shabaya ya malengo ya maendeleo ya millenia.
Ikiwa na kichwa cha habari kisemacho ripoti ya maendeleo ya dunia mwaka 2011, migogoro, usalama na maendeleo, ripoti hiyo imefafanua kuwa ili maeneo hayo yaweza kurejea kwenye mstari wa kawaida yanahitaji taasisi za kiutendaji makini na mifumo ya utawala bora na uwajibikaji.
Kwa mujibu wa rais wa benki hiyo ya dunia Robert, Zoellick amezitolea mwito nchi zilizotumbukia kwenye hali hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia mifumo halisi ya kiutendaji na wakati huo huo kuweka vipaumbele vyenye kupalilia amani na maendeleo.
Ripoti hiyo imeanisha kuwa makundi mengi ya watu duniani bado yanaendelea kuteseka ikiwa ni matokoe ya machafuko na kukosekana kwa ustawi.