Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ITU yahamasisha mabadiliko kutoka utangazaji wa analojia kwenda digitali

ITU yahamasisha mabadiliko kutoka utangazaji wa analojia kwenda digitali

Mkutano wa kimataifa wa teknolojia ya habari na mawasiliano kuhusu kujenga uwezo wa wafanyakazi unafanyika nchini Afrika Kusini ambapo umeangazia zaidi mchakato wa kuhama kutoka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda digitali.

Katika mkutano huo Shirika la mawasilano duniani, ITU limetoa chapisho kuhusu masuala ya digitali na maamuzi yanayopaswa kufanya huku likielimisha washiriki juu ya kipindi hiki cha mpito cha mchakato huo.

Mathalani chapisho hilo linaangalia kwa kina athari za kujengea uwezo wafanyakazi wakati wa kipindi cha mpito na jinsi mashirika na mataifa yanaweza kuandaa watumishi kwa uchumi unaotegemea mfumo wa digitali. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)